Acacia-land English Medium Pre and Primary School

Acacia-land English Medium Pre and Primary School
Acacia-land English Medium Pre and Primary School, P. O. Box 101, Igunga-Tabora. Phone: +255 784 545202

Friday, 29 January 2016

Upaa Vs Busara, Uwezo wa Kitaaluma

 

Kuna dhana kuwa upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya upaa na busara, au uwezo wa kitaaluma. Wanadhana wa dhana hiyo wanaeleza kuwa watu wenye upaa wana busara nyingi na pia uwezo wao wa kitaaluma ni mkubwa. 

Wapo waliokwenda mbali na kusema, si ajabu kuona Maprofesa na Madaktari wa Falsafa wengi wana upaa. Wengine wanaeleza kuwa kunapokuwa na jambo linalohitaji ufumbuzi wa mawazo, pakiwepo watu wawili; mmoja ana upaa na mwingine hana, ikiwa watu hao watatoa mawazo ya ufumbuzi, wazo la mtu mwenye upaa litachukuliwa kwa uzito zaidi.

Hata hivyo dhana hiyo imekua ikipingwa na wataalamu wa maumbile na saikolojia. Wataalamu hao wanaeleza kuwa hakuna uthibitisho wa uhusiano wa moja kwa moja kati ya uwepo wa upaa kwa binadamu na uwezo wa kitaaluma au 'IQ' na/au busara.

Utafiti wa blog hii umegundua uwepo wa baadhi ya watu wenye upaa ambao, kwa kipimo cha kawaida, busara zao zinaweza kutiliwa shaka. Pia wapo wengine ambao hawana kiwango kikubwa cha elimu. Lakini pia tumegundua uwepo wa Maprofesa na Madaktari wa Falsafa wengi ambao hawana upaa. 

Sambamba na hilo, gunduzi nyingi na nadharia mbalimbali zenye mashiko duniani zimefanywa na watu wasiokua na upaa. Mfano: Guru wa Fizikia Sir. Isaac Newton; Guru wa Nuklia Albert Einstein; Guru wa Mahesabu Pythagoras; Maguru wa Falsafa Karl Marx, Plato, Aristotle, Julius Nyerere, n.k.; Baba wa Kompyuta Charles Babbage; Muanzilishi wa Kampuni ya Microsoft Bill Gates; Mvumbuzi katika kampuni ya Apple Steve Jobs; Mvumbuzi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg, na wengine wengi hawana/hakuwa na upaa,

Hata hivyo tuna-'admit' kuwa suala hili linahitaji utafiti zaidi na mjadala mpana. 

Ikiwa dhana hiyo ina ukweli, kuna maswali ya kuvutia ya kitafiti. Mfano: Je, upaa huleta busara, au ni matokeo ya kuwa na busara? na Je, upaa husababisha uwezo mkubwa kitaaluma au uwezo wa kitaaluma husababisha upaa? Maswali haya na mengine mengi yanahitaji majibu.

Thursday, 28 January 2016

Mvua za El Nino zaanza kuleta Maafa Nchini

Mwishoni mwa mwaka jana, Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini ilitoa tahadhari ya mvua za El Nino zilizokuwa zinatarajiwa kunyesha sehemu mbalimbali za nchi. Madhara ya mvua hizo yameanza kujionyesha katika mikoa mbalimbali kama Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Singida, Tabora, Morogoro na kadhalika.

Leo kumekua na taarifa za kuzama kwa kivuko cha mto Kilombero iliyotokea jana jioni. Kivuko hicho kilipinduka na kuzama majini kufuatia mvua iliyoambatana na upepo mkali, na kusababisha maafa na hasara kubwa.

Kivuko cha mto Kilombero baada ya kupata ajali

Kutokea Manyoni, Singida Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Dkt. Kitundu amethibitisha vifo vya watoto wawili waliofariki baada ya kuangukiwa na nyumba kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha wilayani Manyoni

Kwa mujibu wa taarifa ya habari iliyotolewa leo usiku na kituo cha luninga cha ITV, gari aina ya Land Cruiser imesombwa na maji leo mkoani Tabora lilipokua linajaribu kuvuka daraja lililokua limefunikwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha.

Kufuatia matukio haya na mengine mengi, tunatoa wito kuwa sasa ni wakati muafaka kwa kila mtu kuchukua tahadhari kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Tuesday, 26 January 2016

'Computer Arithmetic' Book for Sale!

For those who are interested in learning more about Computer Arithmetic, we've got a very simplified book for you.

This book is comprehensive in its scope, covering basic concepts in computer arithmetic, functionality of computer computations and the role of computer arithmetic in information systems. It also touches on different concepts on number systems.


The book is suitable to undergraduate students in computer science, computer engineering, computer applications, software engineering, and to those preparing for professional examinations in Accountancy, Procurement, Banking and Finance.

For many years the authors of this book have been teaching various computer courses at Universities, thus noted acute shortage of literature on computer written in a language that students can easily understand. Given the poor background of mathematics to most students it becomes imperative to bridge the gap, hence this book.


The book was published in 2014 by the  Dar es Salaam University Press. Please contact me to grab your copy.

Monday, 25 January 2016

Tupate Burudani Kidogo kutoka kwa Yemi Alade

Yemi Alade muimbaji kutoka Nigeria, ametoa toleo la wimbo wake Na Gode kwa Kiswahili. Hii inaonesha jinsi ambavyo kiswahili chetu kinakua. Imagine, from East Africa to West Africa!! Hongera kwa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

Ndani ya wimbo huu utamsikia Yemi akisema "Ukipata usisahau kusema ASANTE KWA MUNGU, lakini pia hata ukikosa usisahau kusema ASANTE kwani bado yeye ni Mungu..." Maneno mujarabu kwelikweli.

Unaweza kusikiliza wimbo huu kwa kubofya PLAY hapa chini.
 


Sunday, 24 January 2016

Rock City - Mwanza

Moja ya vitu ambavyo hupaswi kuvikosa unapotembelea Rock City ni samaki wa kuchoma. Aisee jamaa wako vizuri sana katika kuandaa Sato wa kuchoma. Kingine kizuri ni kuwa utakula Sato aliyevuliwa siku hiyo hiyo yani.


Friday, 22 January 2016

Rais Magufuli ndani ya gwanda za jeshi

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, leo kwa mara ya kwanza ameonekana akiwa ndani ya mavazi rasmi (magwanda) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. 

Rais Magufuli yupo Jijini Arusha ambako, jamoja na mambo mengine, kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.


Thursday, 21 January 2016

Acacialand yafanya kweli matokeo ya Darasa la Nne!

Shule ya Msingi na Awali ya Acacialand (Acacialand Pre and Primary School) yenye mchepuo wa Kiingereza imefanya kweli katika matokeo ya mtihani wa darasa la nne yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kupitia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde. Shule hiyo ni ya Kutwa na Bweni na ipo wilayani Igunga katika mkoa wa Tabora.

Katika Matokeo hayo Acacialand iliyokua na jumla wa watahiniwa 48, imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya (ya kwanza kati ya shule 136), nafasi ya kwanza kimkoa (ya kwanza kati ya shule 764) na nafasi ya 13 kitaifa (ya 13 kati ya shule 16657).  
Sehemu ya wanafunzi wa Acacialand. Ni kama wanasema... "Yeah, our School did it!"
Akizungumza kuhusu matokeo hayo, Mkurugenzi wa Acacialand Mzee Elly Matto, amesema ni matokeo ambayo yamemshangaza kwani alitegemea shule yake ingefanya vizuri lakini hakudhani kama ingekua vizuri kiasi hicho. 

"Mimi nilikua sina taarifa zozote, nimeona tu kwenye taarifa ya habari ya StartTV shule yetu imetajwa kuwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri kitaifa... Tunamshukuru sana Mungu, ametuinua..." alisema Mzee Matto na kuongeza "kutokana na jinsi watoto wetu walivyoandaliwa nilijua tutafanya vizuri, lakini sikutarajia kama tungefanya vizuri kiasi hiki!".

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa changamoto kubwa iliyoko mbele yao kwa sasa ni kuhakikisha kuwa shule inaendelea kufanya vizuri.

Mkurugenzi wa Acacialand Mzee Elly Matto akifanya moja ya majukumu ya Shule akiwa nyumbani
Blog hii ilijitahidi kumtafuta Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Patrick Sagwe ili aeleze nini ilikua siri ya mafanikio kwa shule yake kufanya vizuri ila simu yake muda mwingi ilikua inatumika. Tunaendelea na jitihada za kumtafuta.

Tunapenda kutumia fursa hii kuipongeza Menejimenti ya Shule, Walimu, Wanafunzi na Wafanyakazi wote kwa jitihada kubwa wanayoifanya katika kutoa elimu bora kwa watoto wetu.

>>Unaweza kubofya Hapa au Hapa au Hapa kwa posts zetu zilizopita kuhusu Acacialand. 


Rais Magufuli amteua Rais Mstaafu Kikwete kuwa Mkuu wa UDSM

Rais Magufuli akiwa na Rais Mstaafu Kikwete
Taarifa zilizotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu zinaeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli, amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor of the University of Dar es Salaam).
Uteuzi huo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Balozi Fulgence Kazaura aliyefariki February mwaka 2015.

Kijipu Uchungu Kimeiva!


Tuesday, 19 January 2016

Coming Soon!

Hivi karibuni flyover katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere pale eneo la mataa ya TAZARA itaanza kujengwa. Huu hapa ushahidi.


Monday, 18 January 2016

Message 'Mujarabu'!

It's not how bad you want it, it's about how hard you are willing to work for it! #DeontayWilder

Wednesday, 13 January 2016

Professional Profiles

One of the very important thing that any Professional need is public visibility. This will help him/her to get his/her professional capability known to the public and hence get connections. In this same line, we have decided to publish, from time to time, some of the professional profiles.
Today, we are at the Moshi Co-operative University (MoCU). MoCU, one of the public Universities in Tanzania, is a Center of Excellence in Cooperative Studies and Practices in East Africa. At MoCU we meet Ms. Neema Kumburu. 



Ms. Neema Kumburu is the Associate Dean in the Faculty of Business and Information Studies (FBIS). She is currently finalizing her PhD studies.
 She is young, energetic academician who, apart from management activities, is engaged in teaching, research and consultancy. She has done a number of researches and published enormous research based papers.
Ms. Neema Kumburu