Acacia-land English Medium Pre and Primary School

Acacia-land English Medium Pre and Primary School
Acacia-land English Medium Pre and Primary School, P. O. Box 101, Igunga-Tabora. Phone: +255 784 545202

Friday, 29 January 2016

Upaa Vs Busara, Uwezo wa Kitaaluma

 

Kuna dhana kuwa upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya upaa na busara, au uwezo wa kitaaluma. Wanadhana wa dhana hiyo wanaeleza kuwa watu wenye upaa wana busara nyingi na pia uwezo wao wa kitaaluma ni mkubwa. 

Wapo waliokwenda mbali na kusema, si ajabu kuona Maprofesa na Madaktari wa Falsafa wengi wana upaa. Wengine wanaeleza kuwa kunapokuwa na jambo linalohitaji ufumbuzi wa mawazo, pakiwepo watu wawili; mmoja ana upaa na mwingine hana, ikiwa watu hao watatoa mawazo ya ufumbuzi, wazo la mtu mwenye upaa litachukuliwa kwa uzito zaidi.

Hata hivyo dhana hiyo imekua ikipingwa na wataalamu wa maumbile na saikolojia. Wataalamu hao wanaeleza kuwa hakuna uthibitisho wa uhusiano wa moja kwa moja kati ya uwepo wa upaa kwa binadamu na uwezo wa kitaaluma au 'IQ' na/au busara.

Utafiti wa blog hii umegundua uwepo wa baadhi ya watu wenye upaa ambao, kwa kipimo cha kawaida, busara zao zinaweza kutiliwa shaka. Pia wapo wengine ambao hawana kiwango kikubwa cha elimu. Lakini pia tumegundua uwepo wa Maprofesa na Madaktari wa Falsafa wengi ambao hawana upaa. 

Sambamba na hilo, gunduzi nyingi na nadharia mbalimbali zenye mashiko duniani zimefanywa na watu wasiokua na upaa. Mfano: Guru wa Fizikia Sir. Isaac Newton; Guru wa Nuklia Albert Einstein; Guru wa Mahesabu Pythagoras; Maguru wa Falsafa Karl Marx, Plato, Aristotle, Julius Nyerere, n.k.; Baba wa Kompyuta Charles Babbage; Muanzilishi wa Kampuni ya Microsoft Bill Gates; Mvumbuzi katika kampuni ya Apple Steve Jobs; Mvumbuzi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg, na wengine wengi hawana/hakuwa na upaa,

Hata hivyo tuna-'admit' kuwa suala hili linahitaji utafiti zaidi na mjadala mpana. 

Ikiwa dhana hiyo ina ukweli, kuna maswali ya kuvutia ya kitafiti. Mfano: Je, upaa huleta busara, au ni matokeo ya kuwa na busara? na Je, upaa husababisha uwezo mkubwa kitaaluma au uwezo wa kitaaluma husababisha upaa? Maswali haya na mengine mengi yanahitaji majibu.

No comments:

Post a Comment