Maandalizi ya mbio za Kilimanjaro Marathon zinazofanyika kila mwaka katika siku ya Jumapili ya mwisho ya Mwezi Februari, yanazidi kupamba moto katika viunga mbalimbali vya mji wa Moshi.
Mbio hizo zinazohusisha wanariadha mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zitafanyika Jumapili hii, tarehe 28 February 2016. Waandaaji wa mbio hizo wameeleza kuwa kutakua na mbio za aina tatu: Full Marathon (Kilomita 42), Half Marathon (Kilomita 21), na mbio za kujifurahisha (fun run) za Kilomita tano. Mbio za Kilomita tano zitahusisha pia watu wenye ulemavu.
Mwandishi wetu alifanikiwa kupita katika viunga mbalimbali vya mji wa Moshi na kutupatia pichaz zinazoonesha taswira mbalimbali za maandalizi ya mbio hizo.

Geti kuu la kuingilia katika Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) ambapo shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzia na kumalizia mbio hizo, na sherehe mbalimbali zinazoambatana na mbio hizo zitafanyika |
Sehemu maalumu ya kuanzia na kumalizia mbio hizo ndani ya Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika zikiwa katika maandalizi |
Moja ya mabango yanayohamasisha mbio hizo likiwa katikati ya mji wa Moshi, katika 'Round about' ya mnara wa saa iliyopo karibu na Benki za NBC na CRDB |
Naona maandalizi yanapamba moto..Ata sisi tunakazana na mazoezi ili ata tupate medali.
ReplyDelete