Mwishoni mwa mwaka jana, Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini ilitoa tahadhari ya mvua za El Nino zilizokuwa zinatarajiwa kunyesha sehemu mbalimbali za nchi. Madhara ya mvua hizo yameanza kujionyesha katika mikoa mbalimbali kama Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Singida, Tabora, Morogoro na kadhalika.
Leo kumekua na taarifa za kuzama kwa kivuko cha mto Kilombero iliyotokea jana jioni. Kivuko hicho kilipinduka na kuzama majini kufuatia mvua iliyoambatana na upepo mkali, na kusababisha maafa na hasara kubwa.
Kivuko cha mto Kilombero baada ya kupata ajali |
Kutokea Manyoni, Singida Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Dkt. Kitundu amethibitisha vifo vya watoto wawili waliofariki baada ya kuangukiwa na nyumba kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha wilayani Manyoni
Kwa mujibu wa taarifa ya habari iliyotolewa leo usiku na kituo cha luninga cha ITV, gari aina ya Land Cruiser imesombwa na maji leo mkoani Tabora lilipokua linajaribu kuvuka daraja lililokua limefunikwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha.
Kufuatia matukio haya na mengine mengi, tunatoa wito kuwa sasa ni wakati muafaka kwa kila mtu kuchukua tahadhari kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.
No comments:
Post a Comment