Rais Magufuli akiwa na Rais Mstaafu Kikwete |
Taarifa zilizotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu zinaeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli, amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor of the University of Dar es Salaam).
Uteuzi huo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Balozi Fulgence Kazaura aliyefariki February mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment