Acacia-land English Medium Pre and Primary School

Acacia-land English Medium Pre and Primary School
Acacia-land English Medium Pre and Primary School, P. O. Box 101, Igunga-Tabora. Phone: +255 784 545202

Thursday, 21 January 2016

Acacialand yafanya kweli matokeo ya Darasa la Nne!

Shule ya Msingi na Awali ya Acacialand (Acacialand Pre and Primary School) yenye mchepuo wa Kiingereza imefanya kweli katika matokeo ya mtihani wa darasa la nne yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kupitia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde. Shule hiyo ni ya Kutwa na Bweni na ipo wilayani Igunga katika mkoa wa Tabora.

Katika Matokeo hayo Acacialand iliyokua na jumla wa watahiniwa 48, imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya (ya kwanza kati ya shule 136), nafasi ya kwanza kimkoa (ya kwanza kati ya shule 764) na nafasi ya 13 kitaifa (ya 13 kati ya shule 16657).  
Sehemu ya wanafunzi wa Acacialand. Ni kama wanasema... "Yeah, our School did it!"
Akizungumza kuhusu matokeo hayo, Mkurugenzi wa Acacialand Mzee Elly Matto, amesema ni matokeo ambayo yamemshangaza kwani alitegemea shule yake ingefanya vizuri lakini hakudhani kama ingekua vizuri kiasi hicho. 

"Mimi nilikua sina taarifa zozote, nimeona tu kwenye taarifa ya habari ya StartTV shule yetu imetajwa kuwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri kitaifa... Tunamshukuru sana Mungu, ametuinua..." alisema Mzee Matto na kuongeza "kutokana na jinsi watoto wetu walivyoandaliwa nilijua tutafanya vizuri, lakini sikutarajia kama tungefanya vizuri kiasi hiki!".

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa changamoto kubwa iliyoko mbele yao kwa sasa ni kuhakikisha kuwa shule inaendelea kufanya vizuri.

Mkurugenzi wa Acacialand Mzee Elly Matto akifanya moja ya majukumu ya Shule akiwa nyumbani
Blog hii ilijitahidi kumtafuta Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Patrick Sagwe ili aeleze nini ilikua siri ya mafanikio kwa shule yake kufanya vizuri ila simu yake muda mwingi ilikua inatumika. Tunaendelea na jitihada za kumtafuta.

Tunapenda kutumia fursa hii kuipongeza Menejimenti ya Shule, Walimu, Wanafunzi na Wafanyakazi wote kwa jitihada kubwa wanayoifanya katika kutoa elimu bora kwa watoto wetu.

>>Unaweza kubofya Hapa au Hapa au Hapa kwa posts zetu zilizopita kuhusu Acacialand. 


No comments:

Post a Comment