Acacia-land English Medium Pre and Primary School

Acacia-land English Medium Pre and Primary School
Acacia-land English Medium Pre and Primary School, P. O. Box 101, Igunga-Tabora. Phone: +255 784 545202

Sunday, 28 February 2016

Mbio za Kili Marathon zafana huku Wakenya wakitawala

Mbio za Kilimanjaro Marathon zimefanyika leo katika mji wa Moshi kwa mafanikio makubwa, huku Wakenya wakiendelea kutawala mbio hizo. Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema ikiwa ataendelea kuwa Waziri katika Wizara hiyo, atafanya kila linalowezekana (ila si bao la mkono) kuhakikisha Watanzania pia wanawika katika mbio zijazo.














Picha na Michuzi Blog

Saturday, 27 February 2016

Friday, 26 February 2016

Maandalizi ya Kilimanjaro Marathon 2016 yapamba moto mjini Moshi!

Maandalizi ya mbio za Kilimanjaro Marathon zinazofanyika kila mwaka katika siku ya Jumapili ya mwisho ya Mwezi Februari, yanazidi kupamba moto katika viunga mbalimbali vya mji wa Moshi

Mbio hizo zinazohusisha wanariadha mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zitafanyika Jumapili hii, tarehe 28 February 2016. Waandaaji wa mbio hizo wameeleza kuwa kutakua na mbio za aina  tatu: Full Marathon  (Kilomita 42), Half Marathon (Kilomita 21), na mbio za kujifurahisha (fun run) za Kilomita tano. Mbio za Kilomita tano zitahusisha pia watu wenye ulemavu.

Mwandishi wetu alifanikiwa kupita katika viunga mbalimbali vya mji wa Moshi na kutupatia pichaz zinazoonesha taswira mbalimbali za maandalizi ya mbio hizo. 




Geti kuu la kuingilia katika Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) ambapo shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzia na kumalizia mbio hizo, na sherehe mbalimbali zinazoambatana na mbio hizo zitafanyika

Sehemu maalumu ya kuanzia na kumalizia mbio hizo ndani ya Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika zikiwa katika maandalizi

Mlima Kilimanjaro ukionekana kwa mbali ndani ya uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika, huku mafundi wakiendelea na zoezi la kuandaa maeneo mbalimbali yatakayotumika katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na mbio hizo

Moja ya mabango yanayohamasisha mbio hizo likiwa katikati ya mji wa Moshi, katika 'Round about' ya mnara wa saa iliyopo karibu na Benki za NBC na CRDB

Friday, 29 January 2016

Upaa Vs Busara, Uwezo wa Kitaaluma

 

Kuna dhana kuwa upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya upaa na busara, au uwezo wa kitaaluma. Wanadhana wa dhana hiyo wanaeleza kuwa watu wenye upaa wana busara nyingi na pia uwezo wao wa kitaaluma ni mkubwa. 

Wapo waliokwenda mbali na kusema, si ajabu kuona Maprofesa na Madaktari wa Falsafa wengi wana upaa. Wengine wanaeleza kuwa kunapokuwa na jambo linalohitaji ufumbuzi wa mawazo, pakiwepo watu wawili; mmoja ana upaa na mwingine hana, ikiwa watu hao watatoa mawazo ya ufumbuzi, wazo la mtu mwenye upaa litachukuliwa kwa uzito zaidi.

Hata hivyo dhana hiyo imekua ikipingwa na wataalamu wa maumbile na saikolojia. Wataalamu hao wanaeleza kuwa hakuna uthibitisho wa uhusiano wa moja kwa moja kati ya uwepo wa upaa kwa binadamu na uwezo wa kitaaluma au 'IQ' na/au busara.

Utafiti wa blog hii umegundua uwepo wa baadhi ya watu wenye upaa ambao, kwa kipimo cha kawaida, busara zao zinaweza kutiliwa shaka. Pia wapo wengine ambao hawana kiwango kikubwa cha elimu. Lakini pia tumegundua uwepo wa Maprofesa na Madaktari wa Falsafa wengi ambao hawana upaa. 

Sambamba na hilo, gunduzi nyingi na nadharia mbalimbali zenye mashiko duniani zimefanywa na watu wasiokua na upaa. Mfano: Guru wa Fizikia Sir. Isaac Newton; Guru wa Nuklia Albert Einstein; Guru wa Mahesabu Pythagoras; Maguru wa Falsafa Karl Marx, Plato, Aristotle, Julius Nyerere, n.k.; Baba wa Kompyuta Charles Babbage; Muanzilishi wa Kampuni ya Microsoft Bill Gates; Mvumbuzi katika kampuni ya Apple Steve Jobs; Mvumbuzi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg, na wengine wengi hawana/hakuwa na upaa,

Hata hivyo tuna-'admit' kuwa suala hili linahitaji utafiti zaidi na mjadala mpana. 

Ikiwa dhana hiyo ina ukweli, kuna maswali ya kuvutia ya kitafiti. Mfano: Je, upaa huleta busara, au ni matokeo ya kuwa na busara? na Je, upaa husababisha uwezo mkubwa kitaaluma au uwezo wa kitaaluma husababisha upaa? Maswali haya na mengine mengi yanahitaji majibu.

Thursday, 28 January 2016

Mvua za El Nino zaanza kuleta Maafa Nchini

Mwishoni mwa mwaka jana, Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini ilitoa tahadhari ya mvua za El Nino zilizokuwa zinatarajiwa kunyesha sehemu mbalimbali za nchi. Madhara ya mvua hizo yameanza kujionyesha katika mikoa mbalimbali kama Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Singida, Tabora, Morogoro na kadhalika.

Leo kumekua na taarifa za kuzama kwa kivuko cha mto Kilombero iliyotokea jana jioni. Kivuko hicho kilipinduka na kuzama majini kufuatia mvua iliyoambatana na upepo mkali, na kusababisha maafa na hasara kubwa.

Kivuko cha mto Kilombero baada ya kupata ajali

Kutokea Manyoni, Singida Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Dkt. Kitundu amethibitisha vifo vya watoto wawili waliofariki baada ya kuangukiwa na nyumba kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha wilayani Manyoni

Kwa mujibu wa taarifa ya habari iliyotolewa leo usiku na kituo cha luninga cha ITV, gari aina ya Land Cruiser imesombwa na maji leo mkoani Tabora lilipokua linajaribu kuvuka daraja lililokua limefunikwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha.

Kufuatia matukio haya na mengine mengi, tunatoa wito kuwa sasa ni wakati muafaka kwa kila mtu kuchukua tahadhari kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Tuesday, 26 January 2016

'Computer Arithmetic' Book for Sale!

For those who are interested in learning more about Computer Arithmetic, we've got a very simplified book for you.

This book is comprehensive in its scope, covering basic concepts in computer arithmetic, functionality of computer computations and the role of computer arithmetic in information systems. It also touches on different concepts on number systems.


The book is suitable to undergraduate students in computer science, computer engineering, computer applications, software engineering, and to those preparing for professional examinations in Accountancy, Procurement, Banking and Finance.

For many years the authors of this book have been teaching various computer courses at Universities, thus noted acute shortage of literature on computer written in a language that students can easily understand. Given the poor background of mathematics to most students it becomes imperative to bridge the gap, hence this book.


The book was published in 2014 by the  Dar es Salaam University Press. Please contact me to grab your copy.