Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama akionyesha ujembe wenye maneno "Turudishieni Mabinti Zetu". Michelle alituma picha hii kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter |
Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama, ameungana na jamii ya kimataifa katika kampeni ya kushinikiza kuachiliwa huru kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 200 waliotekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria. Utekaji huo ulifanyika walipokuwa shuleni kwao, kaskazini mwa Nigeria katika mji wa Chibok, April 15 mwaka huu.
Hata hivyo kiongozi wa Boko Haram mapema wiki hii aliachia video inayomuonesha akisema kuwa anakusudia kuwauza hao wasichana kwakua ameagizwa na Allah kufanya hivyo. Katika vido hiyo inayomuonesha akiongea kwa kujiamini huku akitabasamu, kiongozi huyo amesema atawauza mabinti hao, kwani kuna masoko ya kuuzia watu na ni ruhusa kwa wanawake kuuzwa.
Watu mbalimbali ndani na nje ya Nigeria wamelitaka kundi hilo kuwaachilia huru watoto hao, kwani ni haki yao ya msingi kupata elimu na huduma nyingine za kijamii.

Jengo la shule ya Chibok, inayomilikiwa na Serikali, ambapo utekaji huo ulitokea |
No comments:
Post a Comment