Acacia-land English Medium Pre and Primary School

Acacia-land English Medium Pre and Primary School
Acacia-land English Medium Pre and Primary School, P. O. Box 101, Igunga-Tabora. Phone: +255 784 545202

Friday, 14 March 2014

Tunawatakia uchaguzi wa amani Kalenga

Bw. Godfrey Mgimwa, mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi

Bi. Grace Tendega, mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 
Imebaki siku moja kwa kampeni za uchaguzi katika jimbo la uchaguzi la Kalenga kuhitimishwa. Uchaguzi umepangwa kufanyika siku ya Jumapili, tarehe 16/03/2014. Uchaguzi huu unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Dr. Mgimwa. Katika uchaguzi huo vyama viwili ya siasa, CCM kilichomsimamisha Bw. Godfrey Mgimwa, ambaye pia ni mtoto wa marehemu Dr. Mgimwa aliyekua mbuge wa jimbo hilo, na CHADEMA kilichomsimamisha Bi. Grace Tendega vimeonekana kuwa na guvu zaidi ya ushawishi.

Wananchi wamesikiliza kampeni za vyama vyote na wakati wao wa kuamua umefika. Tunaomba maamuzi ya wananchi yaheshimiwe ili kuwe na uchaguzi ulio huru, wa amani na wa haki.

Aidha tunaimani kuwa vyama vyote vitakuwa tayari kuyakubali matokeo kwa mujibu wa wananchi watakavyoamua.

Tunaamini pia kuwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa, kama lilivyotoa tamko lake kwa vyombo vya habari, limejipanga kuhakikisha zoezi la upigaji kura halitawaliwi na mizengwe ya aina yoyote.

Tunatoa pia rai kwa Tume ya Uchaguzi kufanya kazi yao kwa maadili na uzalendo.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Kalenga! 


No comments:

Post a Comment