Watalii wa ndani Bwana Johnes Mwita na Cyril Ochola (Buda) wakifurahia mandhari safi ya maporomoko ya maji ya Marangu |
Wikiendi iliyopita nilikuwa katika mkahawa mmoja katika mji
wa Lilongwe kwa ajili ya chakula. Alikuja bwana mmoja, kijana wa makamo,
tukakaa nae na kuanzisha mazungumzo.
Yeye alinieleza kuwa anafanya kazi katika shirika moja
lilopo katika mji wa Blantyre, kama kilomita 360 hivi kutoka Lilongwe. Katika
kipindi hiki alikua katika likizo yake ya mwaka.
Kitu kilichonifurahisha kwa yule bwana ni kwamba alikuja
Lilongwe kufanya utalii wa ndani. Yeye anasema hutumia likizo yakekutembelea
miji na maeneo mbali mbali ya nchi yake. Likizo hii alikua anatembelea vyo
vikuu vilivyopo Malawi. Alikuwa akienda katika kila chuo ili kujionea
mabadiliko na maendeleo yake.
Nilivutiwa na uamuzi wake, nikawa najiuliza hivi kwetu
Tanzania mambo haya yapo? Utakuta mtu anakaa Dar es Salaam lakini hajawahi hata
kufika Kibaha, achilia mbali Bagamoyo na Zanzibar. Au mtu yupo Moshi lakini
hajawahi kufika pale Marangu Waterfall au hata kufika tu kwenye geti la KINAPA!
Mwingine yupo Arusha lakini hata Arusha National Park hajui pako wapi achilia
mbali maeneo mengine madogo madogo kama Snake Park. Na maeneo mengineyo kadha
wa kadha katika nchi yetu.
Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali. Kuna watu
wanasafiri kutoka maeneo mbalimbali ya dunia kuja kuona Simba wa Serengeti,
twiga wa pale Mikumi, kupanda mlima Kilimanjaro au kutembelea Ngorongoro
Crater. Watu hawa hutumia maelfu ya dola. Lakini maeneo haya na mengine mengi
yapo nchini kwetu, yanatuzunguka, ila hatushawishiki kuyatembelea.
No comments:
Post a Comment