Acacia-land English Medium Pre and Primary School

Acacia-land English Medium Pre and Primary School
Acacia-land English Medium Pre and Primary School, P. O. Box 101, Igunga-Tabora. Phone: +255 784 545202

Wednesday, 26 March 2014

Malawian Airlines yazinduliwa rasmi leo




Shirika la Malawi kwa kushirikiana na Ethiopian Airways leo limezindua rasmi ndege mpya za Malawian Airlines. Malawian Airlines imekuja baada ya Air Malawi kushindwa kufanya vizuri kwenye soko na hivyo kupotea. Malawian Airline inamilikiwa na Seikali ya Malawi pamoja na Ethiopian Airways yenye 49% ya hisa zote.

Rais wa Malawi, Dr. Joyce Banda ndie aliyekuwa mgeni rasmi katika shughuli hii ya leo. Uzinduzi huu ni hatua kubwa na muhimu kwa sekta ya usafirishaji Malawi, na ni funzo kwa mashirika mengine yanayosuasua kama Air Tanzania.

Friday, 21 March 2014

Ukarabati wa milango iliyovunjwa na wezi umeanza







Weekend starts here.


Ijumaa ya leo sio nzuri hapa LUANAR!

Usiku wa kuamkia leo, ijumaa, wezi waliingia kwenye ofisi za Kituo Cha Utafiti na Maendeleo ya Kilimo (Centre for Agricultural Research and Development (CARD)) cha hapa Chuo Kikuu Cha Lilongwe cha Kilimo na Rasilimali Asilia (LUANAR) kilichopo Lilongwe, Malawi. Walipofika waliwafunga kwa kamba walinzi na kuwatupa msituni kisha kuvunja milango ya baadhi ya ofisi na kuingia ndani.

Wameiba baadhi ya vitu na nyaraka mbalimbali, vikiwemo laptops, projectors, flash disks, spika za computer na fedha taslimu (kwenye ofisi ya Mhasibu).

Kilichowashangaza wengi ni kwamba wezi hao wameonekana kuyafahamu vizuri mazingira ya hizi ofisi kiasi cha kujua ni wapi fedha zinawekwa, ni milango ipi inafunguka kirahisi, nakadhalika.

Nilipatwa na mshituko kidogo nilipofika ofisini leo asubuhi nikakuta watu wamejaa na kuna askari wanarandaranda kwenye hizo ofisi. Sikujua kilichotokea mara moja, ila mmoja wa wafanyakazi wa hapa aliniambia hauruhusiwi kuingia ofisini kwako kwa sasa. Nilipomuuliza kulikoni ndipo nilipofahamu mkasa mzima. 

Bahati mbaya ofisi yangu pia ilivunjwa mlango na wezi hao waliingia ndani. Bahati nzuri kwangu sikua nimeacha kitu chochote cha thamani ofisini zaidi ya desktop computer ya ofisi na baadhi ya vitabu. Hata hivyo wezi hao hawakuiba hiyo computer. Nilikuta tu wamefungua droo za meza na za kabineti la kuwekea nyaraka mbalimbali. Sikujua walikua wanatafuta nini, au wameiba nini humo kwenye kabineti maana sikuwahi kulifungua na hivyo sikujua ndani yake kulikua na nini. Polisi walinihitaji kutoa maelezo, na hicho ndicho kimsingi nilichosema.

Inawezekana lile tatizo la umaskini ndio linalochangia vitendo kama hivi kuendelea kutokea.
  


Vitasa vya mlango wa ofisini kwangu vikiwa vimevunjwa na wezi hao

Droo ya cabinet la kuhifadhia nyaraka ikiwa imefunguliwa na wezi hao

Droo za meza na cabinet kwenye ofisi ya jirani yangu Dr. Jumbe zikiwa zimefunguliwa

Droo za cabinet kwenye ofisi ya Bw. Richard Kachule zikiwa zimevunjwa baada ya majaribio ya kuzifungua 'kwa amani' kushindikana

Nyaraka mbalimbali zikiwa zimetawanywa chini kwenye mojawapo ya ofisi

Thursday, 20 March 2014

Cheka, Ongeza Maisha!

MTOTO: baba unaitwa shule
BABA: kuna nini?
MTOTO: sijui, we twende
BABA: haya hebu twende

MWL: karibu mzee, mwanao tumemuuliza Kampala iko wapi kashindwa kujibu
BABA: kamgeukia mwanae akamzaba kibao kwa hasira na kumwambia... wewe nilikukataza kuchezea vitu vya watu, haya KAMPALA ya mwalimu iko wapi?

Nsima Chambo