Wameiba baadhi ya vitu na nyaraka mbalimbali, vikiwemo laptops, projectors, flash disks, spika za computer na fedha taslimu (kwenye ofisi ya Mhasibu).
Kilichowashangaza wengi ni kwamba wezi hao wameonekana kuyafahamu vizuri mazingira ya hizi ofisi kiasi cha kujua ni wapi fedha zinawekwa, ni milango ipi inafunguka kirahisi, nakadhalika.
Nilipatwa na mshituko kidogo nilipofika ofisini leo asubuhi nikakuta watu wamejaa na kuna askari wanarandaranda kwenye hizo ofisi. Sikujua kilichotokea mara moja, ila mmoja wa wafanyakazi wa hapa aliniambia hauruhusiwi kuingia ofisini kwako kwa sasa. Nilipomuuliza kulikoni ndipo nilipofahamu mkasa mzima.
Bahati mbaya ofisi yangu pia ilivunjwa mlango na wezi hao waliingia ndani. Bahati nzuri kwangu sikua nimeacha kitu chochote cha thamani ofisini zaidi ya desktop computer ya ofisi na baadhi ya vitabu. Hata hivyo wezi hao hawakuiba hiyo computer. Nilikuta tu wamefungua droo za meza na za kabineti la kuwekea nyaraka mbalimbali. Sikujua walikua wanatafuta nini, au wameiba nini humo kwenye kabineti maana sikuwahi kulifungua na hivyo sikujua ndani yake kulikua na nini. Polisi walinihitaji kutoa maelezo, na hicho ndicho kimsingi nilichosema.
Inawezekana lile tatizo la umaskini ndio linalochangia vitendo kama hivi kuendelea kutokea.
Vitasa vya mlango wa ofisini kwangu vikiwa vimevunjwa na wezi hao |
Droo ya cabinet la kuhifadhia nyaraka ikiwa imefunguliwa na wezi hao |
Droo za meza na cabinet kwenye ofisi ya jirani yangu Dr. Jumbe zikiwa zimefunguliwa |
Droo za cabinet kwenye ofisi ya Bw. Richard Kachule zikiwa zimevunjwa baada ya majaribio ya kuzifungua 'kwa amani' kushindikana |
Nyaraka mbalimbali zikiwa zimetawanywa chini kwenye mojawapo ya ofisi |
No comments:
Post a Comment