Acacia-land English Medium Pre and Primary School

Acacia-land English Medium Pre and Primary School
Acacia-land English Medium Pre and Primary School, P. O. Box 101, Igunga-Tabora. Phone: +255 784 545202

Monday, 5 May 2014

Safari ya Basi kutoka Lilongwe hadi Dar - Sehemu ya Kwanza

Niliwahi kupata bahati ya kusafiri kwa basi kati ya Lilongwe, Malawi na Dar es Salaam, Tanzania. Ilituchukua jumla ya masaa 30 kusafiri kutoka Lilongwe hadi Dar. Kimsingi ilikua ndio safari yangu ya kwanza ndefu kiasi hicho kusafiri kwa basi.

Safari ilianzia Devil Street, Lilongwe saa moja kamili jioni (kwa saa za Malawi, sawa na saa mbili usiku kwa saa za Tanzania) kwa basi la kampuni ya TAQWA. Kilichonifurahisha wakati wa kuanza safari ni imani waliyonayo Wamalawi kwa Mungu kwani safari yetu ilianza kwa sala. In fact, nimewahi kupata fursa ya kuhudhuria mikutano na vikao kadhaa vya kiofisi nchini Malawi, tena ni vya kiserikali, ambapo asilimia kubwa ya vikao hivyo vilikuwa vikifunguliwa kwa sala! Nchini kwetu vikao vinavyofunguliwa kwa sala labda ni vya taasisi za kidini.
Basi la kampuni ya TAQWA tulilosafiri nalo

Kitu nilichogundua haraka haraka ni kuwa wengi wa abiria waliokua kwenye TAQWA walikua wafanyabiashara. Wanachukua mzigo Dar (hasahasa kariakoo) wanapeleka Malawi. Walikuwemo wafanyabiashara wa kitanzania na kimalawi. Nikagundua kumbe raia wa nchi hizi mbili wana uhusiano mzuri wa kibiashara.

Kituo cha kwanza kusimama kilikua katika hoteli ya Seven Eleven iliyopo katika jiji la Lilongwe. Pale tulisimama kwa ajili ya kununua chakula. Ni ruhusa kwa magari ya abiria kusafiri usiku katika nchi ya Malawi, kwa maana nyingine safari ni masaa 24. 

Baada ya abiria kujinunulia vyakula vyao kwa ajili ya usiku ule, safari ilianza tena kwenye saa mbili kasorobo hivi za Malawi. Tulifika Mzuzu kwenye saa saba za usiku ambapo basi lilisimama kupakia abiria wengine waliokua wakielekea Tanzania.Nakumbuka kabla ya kufika Mzuzu tulisimamishwa njiani na askari kama mara mbili tu.

Baada ya Mzuzu hali ilibadilika. Ilikua ni mwendo wa kukutana na mageti ya askari wa uhamiaji. Kuna mahali tulisimamishwa, usiku huo, tukaamrishwa wote tushuke chini ili wakague hati zetu za kusafiria (Passport). Ilikua ni usiku sana, halafu ni porini na mahali pale palikua na baridi kali sana. Abiria waliwaomba askari hao waingie kukagua hizo hati ndani ya gari kwa maelezo kuwa nje hapakuwa na usalama wa kutosha na pia kulikua na baridi sana.

Askari walivosikia vile wakamuamrisha dereva kuzima gari, na kutueleza kuwa kama hamtaki kushuka mtalala hapahapa. Abiria walijaribu kuweka mgomo wa kushuka lakini askari hawakuwaelewa. Baada ya dakika kama 15 hivi tuliamua kushuka huku abiria wakiwatolea wale askari maneno makali. Kuna mama mmoja, mmalawi, alisikika akisema (kwa Kichewa), "nyie askari wa Malawi mnapenda sana kuabudiwa, nendeni Tanzania mkajifunze kwa wenzenu... sisi sio wahamiaji haramu, ni Wamalawi wenzenu kwanini mnatutesa na baridi hivi usiku huu..?". Mwanaume mwingine mtanzania yeye ndio kidogo alete tafrani. Aliwaambia wale askari kwa Kiswahili (sijui alikua anafikiri hawajui Kiswahili au aliamua tu kusema ili liwalo na liwe), "...mnashindwa  kulala makwenu mnakuja kukesha huku porini... nchi yenyewe maskini, haina tembo, haina almasi, haina dhahabu, haina rasilimali zozote... mtu atakuja kuzamia huku kutafuta nini... wenzenu wanatafuta kuungana nyie mnatafuta kujitenga!..."  Kuna askari mmoja alikua juu ya gari (Pick up) akayasikia yale maneno, aliruka chini kama mshale kuja kumkamata yule bwana, ila abiria kwa umoja wao walimzingira yule askari wakimzuia asimkamate. Mwishowe askari akaona isiwe taabu akaachana nae.

Zoezi la ukaguzi wa Passport lilikua la abiria mmoja baada ya mwingine, ukishakaguliwa ndio unaruhusiwa kuingia ndani ya gari. Baada ya hilo zoezi safari iliendelea, ila kama kawaida mageti ya ukaguzi yalikua mengi japo hatukuwahi tena kushushwa chini. Safari iliendelea mpaka tulipofika Songwe, mpakani mwa Malawi na Tanzania kwenye saa kumi na mbili kasorobo hivi alfajiri kwa masaa ya Tanzania.

Geti la mpakani upande wa Malawi likiwa bado limefungwa, asubuhi hiyo

Basi tulilokuwa tukisafiri nalo likisubiri geti la mpakani lifunguliwe
Magari mengine yakiwa mpakani upande wa Malawi yakisubiri geti la mpaka lifunguliwe
Itaendelea Sehemu ya Pili.....

J. K. Nyerere

Huyu mzee alikua anaheshimika sana. Tazama walivoweka mikono nyuma wakati wanaongea nae! He is real a Father of our Nation..

Friday, 2 May 2014

30 Quotes to help you let go, and continue with your life...

Guys,

Letting go doesn’t mean you don’t care about someone or something anymore; it’s just realizing that the only thing you truly have control over is yourself, right here, right now.  It’s a necessary process of adapting to the ever-changing realities of life – leaving behind the past to make way for the present.

Here are 30 quotes that will help you let go and live well.
  1. You will never achieve what you are capable of if you’re too attached to things you’re supposed to let go of.
  2. Sometimes there are things in our lives that aren’t meant to stay.  Sometimes the changes we don’t want are the changes we need to grow.
  3. Growth and change may be painful sometimes, but nothing in life is as painful as staying stuck where you don’t belong.
  4. Don’t be afraid of change.  Change happens for a reason.  Roll with it.  It won’t be easy, but it will be worth it.
  5. It’s usually quite hard to let go and move on, but once you do, you’ll feel free and realize it was the best decision you’ve ever made.
  6. Never let your fear decide your future.
  7. Fear doesn’t exist anywhere except in your mind.  It’s difficult to follow your heart, but it’s a tragedy to let the lies of fear stop you. 
  8. One of the most rewarding moments in life is when you finally find the courage to let go of what you can’t change.
  9. Never force anything. If it’s meant to be, it will be.  Don’t hold yourself down with things you can’t control.
  10. Live simply.  Love generously.  Speak truthfully.  Breathe deeply.  Do your best.  Leave everything else to the powers above you.
  11. Moving on doesn’t mean forgetting, it means you choose happiness over hurt.
  12. Giving up doesn’t always mean you’re weak; sometimes it simply means you are strong enough to let go.
  13. Whatever is bringing you down, let it GO!  You don’t need that negativity in your life.  Keep calm and be positive.  Good things will happen.
  14. Some people cannot stand that you’re moving on with your life and so they will try to drag your past to catch up with you.  Do not help them by acknowledging their behaviour.  Keep moving forward.
  15. Love yourself!  Forgive yourself!  Accept yourself!  You are YOU and that’s the beginning and the end - no apologies, no regrets.
  16. You are GOOD enough, SMART enough, FINE enough, and STRONG enough.  You don’t need other people to validate you; you’re already valuable. 
  17. Try not to take things other people say about you too personally.  What they think and say is a reflection of them, not you.
  18. If you care too much about what other people think and say about you, in a way, you will always be their prisoner.
  19. Not everyone will appreciate what you do for them.  You have to figure out who’s worth your attention and who’s just taking advantage of you.
  20. Saying yes to happiness means learning to say no to the people and things that hurt you.  Be wise enough to walk away from the negativity.
  21. What you allow is what will continue.  It’s better to be lonely than allow negative people and their opinions derail you from your destiny.
  22. If you feel like your ship is sinking, it might be a good time to throw out the stuff that’s been weighing it down.  Let go of people or things which bring you down, and surround yourself with those who bring out the best in you.
  23. The first to apologize is the bravest.  The first to forgive is the strongest.  The first to move forward is the happiest.
  24. Don’t cry over the past, it’s gone.  Don’t stress about the future, it hasn’t arrived.  Do your best to live in the NOW and make it beautiful.
  25. Life is too short to spend at war with yourself.  Practice acceptance and forgiveness.  Letting go of yesterday’s troubles is your first step towards happiness today.
  26. Old worries are down payments on problems you may never have.  Let them go.  Today is a NEW beginning; take a deep breath and START AGAIN.
  27. Smile, even when it feels like things are falling apart.  Smiling doesn’t always mean you’re happy; sometimes it simply means you’re strong.
  28. There comes a time when you have to stop thinking about your mistakes and move on.  No regrets in life – just lessons that show you the way.
  29. You can’t let one bad moment spoil a bunch of good ones.  Don’t let the silly little dramas of each day get you down.
  30. If you are diligent and patient, everything you truly need in your life will come to you at the right time.