Acacia-land English Medium Pre and Primary School

Acacia-land English Medium Pre and Primary School
Acacia-land English Medium Pre and Primary School, P. O. Box 101, Igunga-Tabora. Phone: +255 784 545202

Wednesday, 9 April 2014

Huyu ndie Jose Mourinho 'The Happy One'

Pamoja na kipigo cha 3-1 alichokipata meneja wa Chelsea Jose Mourinho wiki iliyopita nchini Ufaransa kutoka kwa PSG, timu yake ya Chelsea imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya UEFA baanda ya jana usiku kuichakaza PSG magoli 2-0. 

Chelsea wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya wastani wa magoli kuwa 3-3, lakini kwa vile wao walifunga bao moja katika kipigo cha 3-1 nchini Ufaransa wameweza kufuzu hatua ya nusu fainali.

Wafungaji katika mechi ya jana walikua ni Mjerumani Andre Schurrle katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza na Msenegal Demba Ba katika dakika ya 87.

Kujua alichokisema Mourinho baada ya kipigo cha wiki iliyopita gonga hapa>>

Mabomu mawili kati ya haya matatu aliyoyatega Morinho yalilipuka na kusababisha maangamizi kwa PSG

No comments:

Post a Comment