Hii picha hapa chini inaonesha matazamio ya matendo yanayotakiwa kufanywa na watu wenye makundi mbalimbali ya umri (age groups). Jiulize je, unafanya sawasawa na umri wako?
1. Je, bado una michezo ya kitoto wakati umri huo umeshapita?
2. Je, umehitimu shule/chuo katika umri unaotakiwa?
3. Je, umeoa/kuolewa katika umri stahiki?
4. Je, umepata mtoto katika umri muafaka?
5. Je, unafanya kazi za uzalishaji mali katika wakati muafaka?
6. Je, umestaafu katika umri sahihi?
7. Je, umezeeka katika umri unaotakiwa?
Tuesday, 29 April 2014
Monday, 28 April 2014
Mahakama ya kuku
Ukienda katika masoko mengi siku hizi panapouzwa kuku utapata pia huduma ya kuchinjiwa na kunyonyolewa kuku wako. Hizi picha ni katika soko la Shekilango, Dar ambapo vijana hawa walikutwa na kamera yetu wakiwa bize na ajira yao ya kuchinja na kunyonyoa kuku wa wateja wao.
Friday, 11 April 2014
Rais Kikwete atunukiwa tuzo ya uongozi
Rais Jakaya Kikwete |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika
katika sherehe kubwa iliyofanyika Washington nchini Marekani.
Jarida la African Leadership Magazine ambalo huchapishwa mjini London, Uingereza na mjini Washington nchini Marekani, lilimchagua Rais Kikwete kushinda Tuzo hiyo kwa mwaka 2013 baada ya wasomaji na wadau wake wengine wa Jarida hilo kuwa wamemchagua kwa njia ya kura ya maoni Rais Kikwete kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya wananchi wake katika Bara la Afrika.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Tuzo hiyo kwa Mheshimiwa Membe, Balozi Adefuye wa Nigeria katika Marekani amemwelezea kwa undani anavyomfahamu Rais Kikwete akisisitiza kuwa kiongozi huyo wa Tanzania ni kielelezo cha rika jipya la viongozi wa Afrika ambao dira na visheni yao ni maendeleo ya Bara la Afrika na wananchi wake.
Aidha, akizungumza katika hotuba yake ya utangulizi mwanzoni wa sherehe hiyo, Mchapishaji wa Jarida la African Leadership Magazine, Dkt. Ken Giami ameeleza jinsi Rais Kikwete alivyochaguliwa kwa kishindo na wasomaji na wadau wengine wa Jarida hiyo kutokana na mafanikio yake katika uendeshaji na utawala bora wa Tanzania pamoja na mafanikio yake katika ustawi wa kiuchumi wa wananchi wa Tanzania.
Chanzo: BBC Swahili
Wednesday, 9 April 2014
Huyu ndie Jose Mourinho 'The Happy One'
Chelsea wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya wastani wa magoli kuwa 3-3, lakini kwa vile wao walifunga bao moja katika kipigo cha 3-1 nchini Ufaransa wameweza kufuzu hatua ya nusu fainali.
Wafungaji katika mechi ya jana walikua ni Mjerumani Andre Schurrle katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza na Msenegal Demba Ba katika dakika ya 87.
Kujua alichokisema Mourinho baada ya kipigo cha wiki iliyopita gonga hapa>>
Mabomu mawili kati ya haya matatu aliyoyatega Morinho yalilipuka na kusababisha maangamizi kwa PSG |
Monday, 7 April 2014
Ridhiwani Kikwete aibuka kidedea Chalinze
MATOKEO rasmi ya Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze yametangazwa ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata jumla ya kura 20812, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kikipata kura 2628 na chama cha Wananchi CUF kimepata kura 473, AFP 78 na NRA 59.
Kwa matokeo hayo, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda Kiti cha Ubunge Jimbo la Chalinze kwa asilimia 86.5 kupitia kwa mgombea wake Ridhiwani Kikwete.
Matokeo yenyewe ni kama ifuatavyo...
Friday, 4 April 2014
Cheka, Ongeza Maisha.. (Hii ni kwa hisani ya Mdau Loiruk)
Mume: Hello baby!
Mke: Hello swt!
Mume: nitachelewa kurudi leo
Mke: Nilishajua uko kwa vijinamke vyako, wewe ni mzinzi sana, sijui ilikuaje ukanioa, nakuchukia kama nini? sikupendi! Sikupendi!
Mume: Niko BENKI hapa.
Mke: Haa! Ulijuaje kama sina hela, nitolee laki moja baby, nakupenda sana kuliko roho yangu, nakutengea maji ya kuoga sweety. Usisahau hizo pesa, ninunulie na chpsi kuku, mwaaaa!
Mume: Ni BENKI YA DAMU.
Mke: Waambie wakutoe yote!
Mke: Hello swt!
Mume: nitachelewa kurudi leo
Mke: Nilishajua uko kwa vijinamke vyako, wewe ni mzinzi sana, sijui ilikuaje ukanioa, nakuchukia kama nini? sikupendi! Sikupendi!
Mume: Niko BENKI hapa.
Mke: Haa! Ulijuaje kama sina hela, nitolee laki moja baby, nakupenda sana kuliko roho yangu, nakutengea maji ya kuoga sweety. Usisahau hizo pesa, ninunulie na chpsi kuku, mwaaaa!
Mume: Ni BENKI YA DAMU.
Mke: Waambie wakutoe yote!
Thursday, 3 April 2014
JK na RK: Like father, like son!
Rais, Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi na wanachama wa CCM |
Mtoto wa Rais, Riziwani Kikwete akisalimiana na wananchi na wanachama wa CCM |
Rais, Dr. Jakaya Kikwete akiongea na mwananchi nwenye ulemavu |
Riziwani Kiwete akiongea na mwananchi mwenye ulemavu |
Rais, Dr. Jakaya Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni |
Riziwani Kiwete akihutubia mkutano wa kampeni |
Alichokisema Mourinho kufuatia kipigo cha Chelsea kutoka kwa PSG
Kufuatia kipigo cha 3-1 walichokipata Chelsea jana kutoka kwa Paris Saint-Germain (PSG), haya ndiyo maneno aliyoyasema meneja wa Chelsea José Mourinho akizungumzia mechi ya marudiano itakayochezwa wiki ijayo, Darajani Stamford Bridge:
"We have to play thinking that it's possible. And, to be fair, I don't think Paris think it's over. I don't think they think it's done. They feel they are in a good position but I think they know that it's not over. It's a tough job, not impossible, but difficult."
"We have to play thinking that it's possible. And, to be fair, I don't think Paris think it's over. I don't think they think it's done. They feel they are in a good position but I think they know that it's not over. It's a tough job, not impossible, but difficult."
Meneja wa Chelsea José Mourinho |
Subscribe to:
Posts (Atom)