Ndege ya shirika la ndege la Malaysia aina ya Boeing 777, iliyopotelea hewani wakati inatoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing |
Leo ni siku ya nane tangu ndege ya Shirika la Ndege la
Malaysia aina ya Boeing 777 ipotelee kusikojulikana. Ndege hiyo ilikua ikitoka
Kuala Lumpur kuelekea Beijing ikiwa na jumla ya abiria wapatao 239 pamoja na
wafanyakazi wa ndege.
Shirika la ndege la Malaysia lilisema ndege hiyo namba MH370
ilipotea majira ya saa 8:40 kwa saa Malaysia siku ya Ijumaa baada ya kuondoa Kuala
Lumpur. Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili Beijing China majira ya saa 12:30 kwa
saa za Malaysia.
Maswali mengi yanagubika upoteaji wa ndege hiyo. Baadhi
wanahisi pengine kuna watekaji walikuwa ndani ya ndege na hivyo kuiteka na
kuielekeza wanakojua wao. Hata hivyo wadadisi wa mambo wanaona uwezekano wa
kuwa imetekwa ni mdogo kwasababu ikiwa ilitekwa basi watekaji wangeshaeleza
malengo la utekaji wao.
Aidha kutokana na sababu za kisayansi ndege inapopaa inakuwa
imejazwa mafuta kwa kadiri ya umbali itakaosafiri. Kwakuwa mafuta hayo yana
uzito, pamoja na uzito wa abiria na mizigo ndege hairuhusiwi kutua kabla mafuta
hayo yahajatumika hivyo kupunguza uzito. Ikitua kwa lazima kabla ya mafuta
kupungua, uzito utakua mkubwa na hivyo inaweza kuvunjika vunjika. Uwezekano
pekee wa kutua kabla ya kufika mwisho wa safari ni kumwaga mafuta ikiwa bado
hewani. Sasa kama ilitekwa je ilitua kwa umbali sawa na uliokadiriwa? Kama
sivyo je, walipunguza mafuta?
Kuna wengine wanadhani pengine ilikumbana na kimbunga kikali
ikiwa angani na hivyo kuanguka. Hata hivyo swali linabaki kuwa kama ilianguka,
mbona mabaki yake yametafutwa kwa muda wa zaidi ya wiki sasa hayaonekani?
Watu wa dini wanaweza kuamini labda pengine imenyakuliwa.
Lakini hata hivyo huo sio utaratibu wa Mungu kufanya kazi. Swali linabaki pale
pale, hiyo ndege imepotelea wapi?
Labda tuamini kama wanasayansi wanavyosema kuwa dunia yetu ina nguvu ya uvutano (gravitational force), inayovifanya vitu vyote vinavyorushwa angani kurudi chini ardhini, na labda ndege hiyo ilipaa juu sana mpaka ikavuka eneo la uvutano la dunia na hivyo ikapotelea huko!
Mashirika ya ndege katika ukanda wa Afrika Mashariki kama Precision Air, Kenya Airways, Air Uganda, FastJet, n.k. yanatakiwa kufuatilia kwa makini, kwa lengo la kujifunza, kilichotokea Malaysia. |
No comments:
Post a Comment